Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (E.A.G.T MKIMBIZI BIMA)

BIBLIA INATUFUNDISHA NINI ❓

Mawasiliano 0755844288/0688964004

SOMO; Jinsi NDOA Yako Inavyoweza Kuwa na Furaha

MUNGU  anataka familia (katika NDOA) ziwe na hali gani❓

1 πŸ‘ˆπŸ‘‰MUNGU alianzisha ndoa ya kwanza. Biblia inasema kwamba alimuumba mwanamke wa kwanza na “akamleta kwa mwanamume.” Adamu alifurahi sana, naye akasema hivi: “Hatimaye huyu ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu.” (Mwanzo 2:22, 23) Jambo hilo linaonyesha kwamba MUNGU anataka wale waliofunga ndoa wawe na furaha.

2 πŸ‘ˆπŸ‘‰Cha kusikitisha, leo familia nyingi hazina furaha. Hata hivyo, Biblia ina maagizo  yanayozoweza kumsaidia kila mtu katika familia atimize majukumu yake na kufurahia kuwa pamoja.—Luka 11:28 ,"LAKINI YEYE ALISEMA, AFADHALI, HERI WALISIKAO NENO LA MUNGU NA KULISHIKA ."

MUNGU ANATARAJIA WAUME WAFANYE NINI?
3, 4. (a) Mume anapaswa kumtendeaje mke wake❓ (b) Kwa nini ni muhimu kwa mume na mke kusameheana kwa hiari❓

3 Biblia inasema kwamba mume mzuri anapaswa kumpenda na kumheshimu mke wake. Tafadhali, soma Waefeso 5:25-29.πŸ‘‰Enyi waume, wapendeni wake zenu , kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili take . 26πŸ‘‰ ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27πŸ‘‰ apate kujiletea Kanisa tukufu , lisilo na ila wala kunyanzi wa lo lote kama hayo ; bali liwe takatifu lisilo na mawaa . 28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe . Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe . 29πŸ‘‰ Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote ; Bali huulisha na kuutunza , kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa."πŸ‘‰♥️πŸ‘‰ Sikuzote mume anamtendea mke wake kwa upendo. Pia, anamlinda, anamtunza, na hatafanya jambo lolote la kumuumiza.πŸ‘‚πŸ‘‚πŸ‘ˆ♥️πŸ‘ˆ
♥️
4 Mume anapaswa kufanya nini mke wake akikosea❓ Biblia inawashauri waume hivi: “Endeleeni kuwapenda wake zenu nanyi msiwakasirikie kwa uchungu.” (Wakolosai 3:19) Waume, kumbukeni kwamba ninyi pia hufanya makosa. Ikiwa unataka Mungu akusamehe, unapaswa kumsamehe mke  wako. (Mathayo 6:12, 14, 15) Mume na mke wataifurahia sana ndoa yao ikiwa wanasameheana kwa hiari.
♥️
5. Kwa nini mume anapaswa kumheshimu mke wake❓

5 MUNGU  anatazamia mume ame heshima mke wake. Mume anapaswa kuzingatia mahitaji ya mke wake. Hilo ni jambo zito sana. Ikiwa mume anamtendea vibaya mke wake, MUNGU hatasikiliza sala zake. (1 Petro 3:7 Kadhali ninyi waume , kaeni na wake zenu kwa akili ; na kumpa mke heshima , kama chombo kisicho na nguvu ; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima , kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.") 
πŸ™πŸ‘‰MUNGU♥️ anawathamini watu wote wanaompenda. Hawaoni wanaume kuwa bora kuliko wanawake.
♥️
6. Ni nini maana ya mume na mke kuwa “mwili mmoja”❓ 
πŸ’•
6 Yesu alisema kwamba mume na mke “si wawili tena, bali mwili mmoja.” (Mathayo 19:6 πŸ‘‰Hata wamekuwa si wawili tena , bali mwili mmoja. Basi ailowaunganisha Mungu, mwanafamu asiwatenganishe.") Wanapaswa kuwa waaminifu kwa mmoja na mwenzake. (Methali 5:15-21πŸ‘‰Unywe maji na birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako, 16πŸ‘‰Je❗Chemchemi zako zitawanyike mbali , Na mito ya maji katika njia kuu❓ 17πŸ‘‰Yawe yako mwenyewe peke yako , Wala si ya wageni pamoja nawe. 18πŸ‘‰Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako. 19πŸ‘‰Ni Ayala apendaye na paa apendezaye ; Maziwa take yakutoshe sikuzote ; Na kwa upendo wake ushangilie daima . 20πŸ‘‰Mwanangu❗ Mbona unashangilia Malaya , Na kukikumbatia kifua cha mgeni❓21πŸ‘‰ Kwa maana njia za mwanadamu zi mbele za macho ya BWANA , Na mienendo take yote huitafakari.' 
Waebrania 13:4πŸ‘‰Ndoa na iheshimiwe na watu wote , na malazi yawe safi ; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu.") Mume na mke wanapaswa kutimiziana mahitaji yao ya KUTOMBANA. (1 Wakorintho 7:3-5πŸ‘‰Mume na ampe  mkewe haki yake , na vivyo hivyo Mke na ampe mumewe haki yake. 4πŸ‘‰Mke hana amri juu ya mwili wake , Bali mumewe ; vivyo hivyo Mume hana amri juu ya mwili wake , Bali mkewe .5πŸ‘‰Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda , ili mpate faragha kwa kusali ; mkajiane tena , Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.") Mume anapaswa kukumbuka kwamba “hakuna mtu anayeuchukia mwili wake, bali huulisha na kuutunza.” Hivyo, anapaswa kumpenda na kumtunza mke wake. Zaidi ya yote, mke anahitaji mume wake ampende na kumtendea kwa fadhili.—Waefeso 5:29πŸ‘‰Maana hakuna  mtu anayeuchukia mwili wake po pote ; Bali huulisha na kuutunzs , kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa."
πŸ’•
MUNGU ANATARAJIA WAKE WAFANYE NINI❓
7. Kwa nini familia inahitaji kuwa na kichwa❓
πŸ’•
7 Kila familia inahitaji kuwa na kichwa anayeiongoza ili mambo yafanyike kwa mpango. Biblia inasema hivi katika 1 Wakorintho 11:3: “Kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, nacho kichwa cha mwanamke ni mwanamume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu.”
πŸ’•
8. Mke anawezaje kumwonyesha mume wake heshima❓
πŸ’•
 8 Hata waume hukosea. Lakini ikiwa mke anaunga mkono maamuzi ya mume wake na kushirikiana naye kwa hiari, familia nzima inanufaika. (1 Petro 3:1-6πŸ‘‚ 1πŸ‘‰Kadhalika ninyi wake , watiini waume zenu ; kusudi , ikiwa wako wasioliamini Neno , wavutwe kwa mwenendo wa wake zao , pasipo lile Neno , wavutwe kwa mwenendo wa wake zao , pasipo lile Neno ; 2 πŸ‘‰ wakiutazama mwenendo wenu safi , na wa hofu . 3πŸ‘‰Kujipamba kwenu , kusiwe kujipamba kwa nje , yaani , kusuka nywele ; na kujitia dhahabu , na kuvalia mavazi ; 4πŸ‘‰ Bali kuwe utu wa moyoni usioonekana , katika mapambo yasioharibika ; yaani , roho ya upole na utulivu , iliyo ya thamani kuu mbele za MUNGU. 5πŸ‘‰ Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani , waliomtumaini Mungu , na kuwatii waume zao. ,6,πŸ‘‰Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu , akamwita Beans; nanyi ni watoto wake , mfanyapo mema , wala hamkutishwa kwa hofu yo yote ."  ) Biblia inasema: “Mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.” (Waefeso 5:33 πŸ‘‰ Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe ; wala mke asikose kumshahi mumewe." )
πŸ‘‰ Namna gani ikiwa mume si mwamini❓ Bado mke ana wajibu wa kumheshimu. Biblia inasema hivi: “Ninyi wake, watiini  waume zenu, kusudi , ikiwa wako wasioliamini Neno , wavutwe kwa mwenendo wa wake zao , pasipo lile Neno ; 2 wakiutazama mwenendo wenu Safi , na wa hofu." ( 1 Petro 3 : 1-2) 
πŸ‘‰ Hapa wale Wanaume sio waaminifu , wale wasiotii lile neno, wavutwe bila neno kupitia mwenendo wa wake zao, kwa sababu wameshuhudia kwa macho yao mwenendo wenu ulio safi kiadili pamoja na heshima kubwa. πŸ”΄πŸ™ Mfano mzuri wa mke unaweza kumsaidia mume wake akubali na kuheshimu imani ya mke wake.

9. (a) Mke anapaswa kufanya nini ikiwa hakubaliani na wazo fulani la mume wake❓

πŸ‘‰ (b) Andiko la Tito 2:4, 5, linawashauri wake wafanye nini❓4πŸ‘‰ili wawatie wanawake vijana akili , wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wap ; 5πŸ‘‰ na kuwa wenye kiasi , kuwa  safi , kufanya kazi nyumbani mwao , kuwa wema , kuwatii waume zao wenyewe ; ili neno la MUNGU lisitukanwe" 

9πŸ‘‰ Mke anaweza kufanya nini ikiwa hakubaliani na wazo fulani la mume wake❓ Anaweza kueleza maoni yake kwa heshima. Kwa mfano, wakati  fulani Abrahamu hakupendezwa na maoni ya Sara, lakini MUNGU alimwambia hivi: “Msikilize.” (Mwanzo 21:9-12 πŸ‘‰9 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri , ambaye alimzalia Ibrahimu , anafanya dhihaka . 10πŸ‘‰ Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu , Mfukuze mjakazihuyu na mwanawe , maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu , Isaka. 11πŸ‘‰Na neno Hilo lilikuwa baya Sana machoni pa Ibrahimu , kwa ajili ya mwanawe . 12 πŸ‘‰ MUNGU akamwambia Ibrahimu , Neno hili lisiwe baya machoni pako , kwa ajili ya huyo mwana , na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara , sikiliza saiti yake , kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.")
πŸ‘‰ Mke anapaswa kuunga mkono maamuzi yote ya mume wake ikiwa hayavunji maagizo ya MUNGU katika Neno lake( Biblia.)
πŸ‘‰ (Matendo 5:29....πŸ‘‰Petro na mitume wakajibu , wakisema , Imetupasa kumtii MUNGU kuliko wanadamu.") ; Waefeso 5:24...πŸ‘‰ Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila Jambo.")
πŸ‘‰ Mke bora anatunza familia yake. (Soma Tito 2:4, 5.πŸ‘‰4πŸ’žili wawatie wanawake (#A) vijana akili , (#B) wawapende waume zao , (#C) na kuwapenda watoto wao ; 5πŸ‘‰#D ) na kuwa wenye kiasi , (#E) kuwa Safi , (#F) kufanya kazi nyumbani mwao , (#G)kuwa wema , (#H)kuwatii waume zao wenyewe ;πŸ‘ˆ ILI NENO
LA MUNGU LISITUKANWE.")
πŸ‘‰ Mume na watoto wanapoona akifanya kazi kwa bidii, watampenda na kumheshimu sana.—Methali 31:10, 28.πŸ‘‰10 Mke mwema , ni nani awezaye kumwona❓ Maana kima chake chapita kima cha marijani .πŸ‘‰28 Wanawe huondoka na kumwita heri ; Mumewe naye humsifia na kusema πŸ‘‰ Binti za watu wengi wamefanya mema , Lakini wewe umewapita wote."
πŸ˜€♥️πŸ‘‡
Abrahamu akimsikiliza Sara
Kwa nini Sara ni mfano mzuri kwa wanawake❓
πŸ‘‚
10. Biblia inasema nini kuhusu kutengana na talaka❓
πŸ‘‚
10 Nyakati fulani kuna hali zinazoweza kufanya wenzi wa ndoa watengane au kutalikiana. Hata hivyo, Biblia inasema kwamba “mke hapaswi kutengana na mume wake” na “mume hapaswi kumwacha mke wake.” (1 Wakorintho 7:10, 11) Huenda kwa sababu ya matatizo fulani mazito wenzi wa ndoa wakaamua kutengana, hata hivyo huo ni uamuzi mzito. Namna gani kuhusu talaka❓Biblia inasema kwamba sababu pekee inayoweza kufanya mume au mke watalikiane ni uasherati.—Mathayo 19:9.πŸ‘‰Nami nawaambia ninyi , Kila mtu atakayemwacha mkewe , isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati , akaoa mwingine , azini , naye amwoaye yule aliyeachwa azini."
♥️πŸ™
MUNGU ANATARAJIA WAZAZI WAFANYE NINI❓
1. (Magazine yangu jipya Teleo la 1 bado kuingia sokoniπŸ‘‰ Yesu akiwa na watoto; 2. Baba akijifunza na mtoto wake ( Magazine Toleo la 2 jipya πŸ‘‰ Jifunze Kutoka kwa YESU) bado pia kuingia sokoni
(Magazine yangu jipya Toleo 3πŸ‘‰Yesu ni mfano mzuri kwa kila mshiriki wa familia
πŸ‘‡πŸ‘†#MAGAZINEhizoZIKIINGIAsokoniNitawajulisha

11. Watoto wanahitaji nini kutoka kwa wazazi❓

11 Wazazi, tumieni wakati mwingi iwezekanavyo pamoja na watoto wenu. Watoto wanawahitaji ninyi wazazi zaidi ya kitu kingine chochote, wanahitaji muwafundishe kumhusu MUNGU.—Kumbukumbu la Torati 6: 4-9.πŸ‘‰4 Sikiliza , Ee Israeli ; BWANA , MUNGU wetu , BWANA ndiye mmoja. 5πŸ‘‰Nawe mpende BWANA , MUNGU wako, kwa moyo wako wote , na kwa roho yako yote , na kwa nguvu zako zote . 6πŸ‘‰Na maneno haya ninayokuamuru leo , yatakuwa katika moyo wako . 7πŸ‘‰ nawe wafundishe watoto wako kwa bidii , na kuyanena uketipo katika nyumba yako , itembeapo njiani , na ulalapo , na uondokapo . 8πŸ‘‰ Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako , nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. 9πŸ‘‰Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako , na juu ya malango yako."
πŸ‘‡
12. Wazazi wanapaswa kufanya nini ili kuwalinda watoto wao❓
πŸ‘‡
12 Ulimwengu huu toka kutupwa kwa shetani umekuwa mwovu sana, pia kuna baadhi ya watu ambao wanataka kuwadhuru watoto wetu, kwa kuwatendea vibaya kingono(Sex). Ni vigumu kwa baadhi ya wazazi kuwafundisha watoto  wao kuhusu ngono (Sex). Hata hivyo, wazazi wanapaswa kuwaonya watoto wao kuhusu watu hao wabaya na kuwafundisha jinsi ya kuwaepuka. Wazazi, mnapaswa kuwalinda watoto wenu. *—1 Petro 5:8πŸ‘‰Mwe na kiasi na kukesha ; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi , kama Simba angurumaye , huzunguka -zunguka , akitafuta mtu ammeze."
πŸ‘‡
13. Wazazi wanapaswa kuwafundishaje watoto wao❓
πŸ‘‡
13 Wazazi wana wajibu wa kuwafundisha watoto wao tabia nzuri. Unawezaje kuwafundisha watoto wako tabia nzuri❓ Watoto wako wanahitaji nidhamu, lakini nidhamu haipaswi kutolewa kwa ukatili.  (Yeremia 30:11πŸ‘‰Maana Mimi ni pamoja nawe , asema BWANA , nikuokoe ; maana nitawakomesha kabisa Mataifa yote huko nilikokutawanya , Bali sitakukomesha wewe kabisa ; lakini nitakurudi kwa hukumu , wala sitakuacha bila adhabu .") Kwa hiyo, usimwadhibu mtoto wako unapokuwa na hasira. Usitumie maneno makali ‘yanayochoma kama upanga’ ambayo yatawaumiza. (Methali 12:18 πŸ‘‰Kuna anenaye bila kufikiri , kama kuchoma kwa upanga ; Bali ulimi wa mwenye haki ni Afya .") Wafundishe watoto wako umuhimu wa kutii.—Waefeso 6:4πŸ‘‰Nanyi , akina baba , msiwachokoze watoto wenu ; bali waleeni katika adabu na maonyo ya BWANA."; Waebrania 12:9-11πŸ‘‰9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi , nasi tukawastahi ; basi si atadhali Sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi❓ πŸ‘‰10 Maana ni hakika , hao kwa siku chache waliturudi  kama walivyoona vema wenyewe ; Bali yeye kwa faida yetu , ili tuushiriki utakatifu wake . 11πŸ‘‰ Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha , bali huzuni ; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye Imani."
πŸ‘‡
MUNGU ANATARAJIA WATOTO WAFANYE NINI❓
14, 15. Kwa nini watoto wanapaswa kuwatii wazazi wao❓
πŸ‘‡
14 Yesu alimtii Baba yake sikuzote, hata ilipokuwa vigumu kufanya hivyo. (Luka 22:42; Yohana 8:28, 29) MUNGU anatarajia watoto wawatii wazazi wao.—Waefeso 6:1-3.
πŸ‘‡
15 Watoto, hata mkihisi kwamba ni vigumu kuwatii wazazi wenu, kumbukeni kwamba mkiwa watiifu, mtamfurahisha MUNGU na wazazi wenu. *—Methali 1:8; 6:20; 23:22-25.
πŸ‘‡
Mvulana akipinga kishawishi cha kuvuta sigara kutoka kwa wenzake
Ni nini kitakachowasaidia vijana kumtii Mungu wanaposhawishiwa kufanya mambo mabaya❓
πŸ‘‡
16. (a) Shetani anatumia njia gani kuwashawishi vijana wafanye mambo mabaya❓ (b) Kwa nini ni muhimu kuchagua marafiki wanaompenda MUNGU❓
πŸ‘‡
16 Ibilisi anaweza kuwatumia rafiki zako na vijana wengine ili wakushawishi ufanye mambo mabaya. Anajua kwamba itakuwa vigumu kwako kuwapinga. Kwa mfano, Dina binti ya Yakobo alikuwa na marafiki ambao hawakumpenda Yehova. Urafiki huo ulimletea matatizo mengi sana yeye na pia familia yake. (Mwanzo 34:1, 2) Ikiwa rafiki zako hawampendi Yehova, wanaweza kukushawishi ufanye mambo yanayomchukiza, hivyo kukuumiza wewe, familia yako, na Mungu. (Methali 17:21, 25) Kwa kweli, ni muhimu  kutafuta marafiki wanaompenda Yehova.—1 Wakorintho 15:33.
πŸ‘‡
FAMILIA YAKO INAWEZA KUWA NA FURAHA
17. Kila mtu katika familia ana wajibu gani❓
πŸ‘‡
17 Washiriki wa familia wanapofuata mwongozo wa Mungu, wanaepuka matatizo mengi. Hivyo, ikiwa wewe ni mume mpende mke wako. Mke, unapaswa kumheshimu na kumtii mume wako, pia unapaswa kuiga mfano wa mke anayetajwa katika Methali 31:10-31. Ikiwa wewe ni mzazi, wafundishe watoto wako kumpenda Mungu. (Methali 22:6) Ikiwa wewe ni baba, ongoza familia yako “vizuri.” (1 Timotheo 3:4, 5; 5:8) Nanyi watoto, watiini wazazi wenu. (Wakolosai 3:20) Kumbuka kwamba kila mtu katika familia anaweza kukosea, hivyo uwe mnyenyekevu na kuwaomba wengine msamaha. Naam, Biblia ina mwongozo wa Yehova kwa ajili ya kila mtu katika familia.
πŸ‘‡
HITIMISHO LA SOMO HILIπŸ‘†REFU
UKWELI WA 1: MUNGU  ALIANZISHA FAMILIA
“Kwa sababu hiyo ninampigia Baba magoti, ambaye kila familia mbinguni na duniani hupata jina kutoka kwake.”​—Waefeso 3:14, 15
πŸ‘‡
Jinsi familia yako inavyoweza kuwa na furaha.
πŸ‘‡
Mwanzo 1:26-28
πŸ‘‡
MUNGU  alianzisha familia ya kwanza.
πŸ‘‡
Waefeso 5:1, 2
πŸ‘‡
Siri ya kuwa na maisha ya familia yenye furaha ni kufuata Neno la MUNGU 
πŸ‘†
UKWELI WA 2: JINSI YA KUWA MUME AU MKE BORAπŸ‘‡
“Kila mtu kati yenu anapaswa kumpenda mke wake . . . mke anapaswa kumheshimu sana mume wake.”—Waefeso 5:33
πŸ‘‡
Mume na mke wanapaswa kutendeanaje❓
πŸ‘‡
Waefeso 5:22-29
πŸ‘‡
Mume ni kichwa cha familia. Anapaswa kumpenda mke wake naye mke anapaswa kuunga mkono maamuzi ya mume wake.
πŸ‘‡
Wakolosai 3:19; 1 Petro 3:4
πŸ‘‡
Wanapaswa kutendeana kwa fadhili na ufikirio.
πŸ‘‡
1 Petro 3:1, 2, 7
πŸ‘‡
Mume na mke wanapaswa kuheshimiana.
πŸ‘‡
1 Timotheo 5:8; Tito 2:4, 5
πŸ‘‡
Mume anapaswa kuiandalia familia yake. Mke anapaswa kuitunza nyumba yake kwa njia inayofaa.
πŸ‘‡
 UKWELI WA 3: JINSI YA KUWA MZAZI BORA
Msiwe mkiwakasirisha watoto wenu, bali endeleeni kuwalea katika nidhamu na maagizo ya MUNGU—Waefeso 6:4
πŸ‘‡
Wazazi wana wajibu gani❓
πŸ‘‡
Kumbukumbu la Torati 6:4-9; Methali 22:6
πŸ‘‡
Tenga wakati wa kuwafundisha watoto wako kumhusu Yehova. Anza wakiwa wachanga na uwasaidie kuwa rafiki za Yehova.
πŸ‘‡
1 Petro 5:8
πŸ‘‡
Wafundishe watoto wako jinsi wanavyoweza kuepuka kutendewa vibaya kingono na hatari nyinginezo.
πŸ‘‡
Yeremia 30:11; Waebrania 12:9-11
πŸ‘‡
Unapaswa kuwatia nidhamu watoto wako, lakini si kwa hasira au kwa ukatili.
πŸ‘‡
UKWELI WA 4: MUNGU ANATAZAMIA WATOTO WAFANYE NINI❓
“Enyi watoto, watiini wazazi wenu.”—Waefeso 6:1
πŸ‘‡
Watoto, kwa nini mnapaswa kuwatii wazazi wenu❓
πŸ‘‡
Methali 23:22-25; Wakolosai 3:20
πŸ‘‡
Unapotii utamfurahisha MUNGU na wazazi wako.
πŸ‘‡
1 Wakorintho 15:33
πŸ‘‡
Uwe rafiki wa wale wanaompend MUNGU Hivyo, itakuwa rahisi kwako kutenda mambo mema.

Comments

Popular posts from this blog

SOMO: FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA by 0755844288/0688964004 mpaka whatsapp. FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA. 1. Unakuwa na uhakika wa kusamehewa dhambi zako zote; 1Yohana 2:1-2, 1Yohana 1:8-10, Ufunuo 1:4-5. 2. Unakuwa na uhakika kuwa dhambi zote ulizotubu kwa kumaanisha kuziacha zimesamehewa na kusahauliwa kabisa na Mungu; Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zaburi 103:20. 3. Una uhakika wa kupata nguvu ya kuacha jumla kila dhambi iliyokuwa ikikutesa kabla; Warumi 6:6-11, Warumi 6:12-14, 1Petro 2:24. 4. Unapewa uwezo wa kufanyika kuwa mtoto wa Mungu kisheria; Yohana 1:12, 1Petro 2:9, 1Yohana 3:1-2. 5. Ukiwa na Yesu “tayari” wewe ni mwenyeji wa mbinguni; Waefeso 2:19, 1Petro 2:9, Ufunuo 5:9. 6. Tayari UNA UZIMA WA MILELE ndani yako; Yohana 3:16-18, Yohana 17:3, Yohana 5:24, 1Yohana 5:13. 7. Umebarikiwa tayari kwa baraka zote za rohoni (anazomilki Mungu), na ni zako wewe na Bwana Yesu mnazirithi pamoja. Kila alichonacho Mungu ni chako wewe na Bwana Yesu. Na wewe na Bwana Yesu mna haki sawa mbele za Mungu baba katika kurithi alivyonavyo; Waefeso 1:3, Warumi 8:16-17, Wagalatia 4:6-7. 8. Yesu amekukatia “BIMA YA AFYA” msalabani. Ukiamini ni haki yako KUTOKUWA MGONJWA kabisa; Isaya 53:4-5, 1Petro 2:24, Mathayo 8:16-17, Zaburi 103:3, Isaya 33:20-24, Isaya 35:8-10. 9. Uhakika wa ushindi, uhakika wa nguvu, na uhakika wa mamlaka dhidi ya NGUVU ZOTE ZA GIZA; Wakolosai 1:13, 1Petro 2:9, Yohana 8:12, Isaya 60:1-3, Zaburi 91:2-13, Luka 10:19, Luka 9:1-2, Hesabu 23:23. 10. Uhakika wa ulinzi wa Ufalme wa Mungu kwako; Zaburi 34:7, Zaburi 91:2-13, 1Petro 1:5, Kutoka 23:20. 11. Uhakika wa hatma/ mwisho mwema; Wafilipi 1:6, Wafilipi 2:13, Yeremia 29:11, Mithali 4:18, Ayubu 8:7, Ayubu 42:12-17. 12. Uhakika wa maisha marefu; Yohana 11:25-26, Zaburi 91:14-16, Ayubu 42:16-17, Isaya 65:19-20. 13. Uhakika wa kuweza “kutembea na Mungu” kama best friend wako kila mahali na kila siku, Huku akifanya mambo ya kushangaza kupitia wewe na pamoja na wewe; 1Samweli 3:19, Matendo 10:38, Yohana 3:2, Marko 16:20, Kutoka 33:12-17. 14. Uhakika wa wewe mwenyewe kuwa “ishara na ajabu” kwa kizazi chako na kufanya dunia ijue kwamba ulikuwepo (LEGACY); Isaya 8:18, Marko 16:17-18, 20, Matendo 1:8, Matendo 5:12-16, Matendo 6:8, Matendo 8:5-13, Matendo 19:11-12. Wokovu ni mtamu sana. Ukiokoka, huwezi kuyapata haya katika uhalisia wake mpaka utakapoamua kuwa mtakatifu. Kiwango cha ubora wako kinategemea uamuzi wako wa kuwa MTAKATIFU na kujitenga na dhambi (2Timotheo 2:20-26). Zingatia hili; Usikubali Shetani akudanganye kusoma ujumbe huu bila kusoma na maandiko yaliyomo. Siri kubwa ya kuwa mtu wa imani ni kufuatilia na kusoma maandiko. Hakikisha umeyasoma vizuri na kwa utulivu. KWA WAKAZI WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO MWALIMU KABIGUMILA ATAKUWA HUKO soma tangazo hili chini Mwl Dickson Cornel Kabigumila www.yesunibwana.org 0 MWIMBAJI JOYOUS CELEBRATION AMALIZA MKATABA NA KUMRITHISHA NAFASI YAKE MDOGO WAKE » « SOMO: KUJISHUHUDIA MWENYEWE - ASKOFU KAKOBE Tags: faida za kuokoka na kuamua kuishi maisha matakatifu yasiyo na michanganyo.mwalimu Dickson Kabigumilasomo.neno admin : Related Post From Christmases to Happy Holidays SOMO: KUMPATA BABA ASKOFU AMFUKUZA MFANYAKAZI WA NDANI KWA KUBANIA FUNGU LA KUMI