Posts

Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (E.A.G.T MKIMBIZI BIMA)

BIBLIA INATUFUNDISHA NINI ❓ Mawasiliano 0755844288/0688964004 SOMO ; Jinsi NDOA Yako Inavyoweza Kuwa na Furaha MUNGU  anataka familia (katika NDOA) ziwe na hali gani❓ 1 👈👉MUNGU alianzisha ndoa ya kwanza. Biblia inasema kwamba alimuumba mwanamke wa kwanza na “akamleta kwa mwanamume.” Adamu alifurahi sana, naye akasema hivi: “Hatimaye huyu ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu.” (Mwanzo 2:22, 23) Jambo hilo linaonyesha kwamba MUNGU anataka wale waliofunga ndoa wawe na furaha. 2 👈👉Cha kusikitisha, leo familia nyingi hazina furaha. Hata hivyo, Biblia ina maagizo  yanayozoweza kumsaidia kila mtu katika familia atimize majukumu yake na kufurahia kuwa pamoja.—Luka 11:28 ,"LAKINI YEYE ALISEMA, AFADHALI, HERI WALISIKAO NENO LA MUNGU NA KULISHIKA ." MUNGU ANATARAJIA WAUME WAFANYE NINI? 3, 4. (a) Mume anapaswa kumtendeaje mke wake❓ (b) Kwa nini ni muhimu kwa mume na mke kusameheana kwa hiari❓ 3 Biblia inasema kwamba mume mzuri anapaswa kumpenda na kumheshimu

SOMO: FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA by 0755844288/0688964004 mpaka whatsapp. FAIDA ZA KUOKOKA NA KUAMUA KUISHI MAISHA MATAKATIFU (BILA MICHANGANYO) BAADA YA KUOKOKA. 1. Unakuwa na uhakika wa kusamehewa dhambi zako zote; 1Yohana 2:1-2, 1Yohana 1:8-10, Ufunuo 1:4-5. 2. Unakuwa na uhakika kuwa dhambi zote ulizotubu kwa kumaanisha kuziacha zimesamehewa na kusahauliwa kabisa na Mungu; Isaya 1:18, Isaya 43:25, Zaburi 103:20. 3. Una uhakika wa kupata nguvu ya kuacha jumla kila dhambi iliyokuwa ikikutesa kabla; Warumi 6:6-11, Warumi 6:12-14, 1Petro 2:24. 4. Unapewa uwezo wa kufanyika kuwa mtoto wa Mungu kisheria; Yohana 1:12, 1Petro 2:9, 1Yohana 3:1-2. 5. Ukiwa na Yesu “tayari” wewe ni mwenyeji wa mbinguni; Waefeso 2:19, 1Petro 2:9, Ufunuo 5:9. 6. Tayari UNA UZIMA WA MILELE ndani yako; Yohana 3:16-18, Yohana 17:3, Yohana 5:24, 1Yohana 5:13. 7. Umebarikiwa tayari kwa baraka zote za rohoni (anazomilki Mungu), na ni zako wewe na Bwana Yesu mnazirithi pamoja. Kila alichonacho Mungu ni chako wewe na Bwana Yesu. Na wewe na Bwana Yesu mna haki sawa mbele za Mungu baba katika kurithi alivyonavyo; Waefeso 1:3, Warumi 8:16-17, Wagalatia 4:6-7. 8. Yesu amekukatia “BIMA YA AFYA” msalabani. Ukiamini ni haki yako KUTOKUWA MGONJWA kabisa; Isaya 53:4-5, 1Petro 2:24, Mathayo 8:16-17, Zaburi 103:3, Isaya 33:20-24, Isaya 35:8-10. 9. Uhakika wa ushindi, uhakika wa nguvu, na uhakika wa mamlaka dhidi ya NGUVU ZOTE ZA GIZA; Wakolosai 1:13, 1Petro 2:9, Yohana 8:12, Isaya 60:1-3, Zaburi 91:2-13, Luka 10:19, Luka 9:1-2, Hesabu 23:23. 10. Uhakika wa ulinzi wa Ufalme wa Mungu kwako; Zaburi 34:7, Zaburi 91:2-13, 1Petro 1:5, Kutoka 23:20. 11. Uhakika wa hatma/ mwisho mwema; Wafilipi 1:6, Wafilipi 2:13, Yeremia 29:11, Mithali 4:18, Ayubu 8:7, Ayubu 42:12-17. 12. Uhakika wa maisha marefu; Yohana 11:25-26, Zaburi 91:14-16, Ayubu 42:16-17, Isaya 65:19-20. 13. Uhakika wa kuweza “kutembea na Mungu” kama best friend wako kila mahali na kila siku, Huku akifanya mambo ya kushangaza kupitia wewe na pamoja na wewe; 1Samweli 3:19, Matendo 10:38, Yohana 3:2, Marko 16:20, Kutoka 33:12-17. 14. Uhakika wa wewe mwenyewe kuwa “ishara na ajabu” kwa kizazi chako na kufanya dunia ijue kwamba ulikuwepo (LEGACY); Isaya 8:18, Marko 16:17-18, 20, Matendo 1:8, Matendo 5:12-16, Matendo 6:8, Matendo 8:5-13, Matendo 19:11-12. Wokovu ni mtamu sana. Ukiokoka, huwezi kuyapata haya katika uhalisia wake mpaka utakapoamua kuwa mtakatifu. Kiwango cha ubora wako kinategemea uamuzi wako wa kuwa MTAKATIFU na kujitenga na dhambi (2Timotheo 2:20-26). Zingatia hili; Usikubali Shetani akudanganye kusoma ujumbe huu bila kusoma na maandiko yaliyomo. Siri kubwa ya kuwa mtu wa imani ni kufuatilia na kusoma maandiko. Hakikisha umeyasoma vizuri na kwa utulivu. KWA WAKAZI WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO MWALIMU KABIGUMILA ATAKUWA HUKO soma tangazo hili chini Mwl Dickson Cornel Kabigumila www.yesunibwana.org 0 MWIMBAJI JOYOUS CELEBRATION AMALIZA MKATABA NA KUMRITHISHA NAFASI YAKE MDOGO WAKE » « SOMO: KUJISHUHUDIA MWENYEWE - ASKOFU KAKOBE Tags: faida za kuokoka na kuamua kuishi maisha matakatifu yasiyo na michanganyo.mwalimu Dickson Kabigumilasomo.neno admin : Related Post From Christmases to Happy Holidays SOMO: KUMPATA BABA ASKOFU AMFUKUZA MFANYAKAZI WA NDANI KWA KUBANIA FUNGU LA KUMI